Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DED kortini kesi ya uhujumu uchumi

Hukumu Pc Data DED kortini kesi ya uhujumu uchumi

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewaunganisha washitakiwa wengine saba akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi, Catherine Mashalla katika kesi ya uhujumu uchumi na kufanya idadi ya washitakiwa katika kesi hiyo kufikia 14.

Mashalla ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, ameunganishwa katika shauri hilo namba 5 la mwaka 2023, ambapo wamesomewa mashitaka 153, ikiwemo utakatishaji wa fedha, kuunda genge la uhalifu na kughushi malipo kwa njia ya mtandao kinyume na utaratibu.

Kesi hiyo ilisomwa jana Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rebeca Mwalusako, upande wa Jamuhuri ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa Takukuru, ulieleza kuwa kesi hiyo mara ya kwanza ilitajwa mahakamani hapo Agosti 22, 2023 ikiwakabili washitakiwa saba.

Baada ya kusomewa mashtaka watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa vile mahakama hiyo haina mamlaka ya kuendesha kesi za uhujumu uchumi. Kesi imeahirishwa hadi Machi 28, mwaka huu itakapotajwa tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live