Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DCI Wambura "Wahalifu tafuteni kazi ingine hatuna huruma kwenu"

Wambu 660x400.jpeg DCI Wambura "Wahalifu tafuteni kazi ingine hatuna huruma kwenu"

Sat, 12 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camilius Wambura amesema Jeshi la Polisi halitamvumilia mtu yeyote atakayeendelea kujihusisha na vitendo vya uhalifu, kauli ambayo ameitoa  wakati huu ambao Jeshi hilo linaendelea na operesheni kali ya kupambana na vitendo hivyo.

DCI Wambura ameyasema hayo leo Jijini Dodoma katika kikao kazi kilichowashirikisha Maofisa wa Makao Makuu ya Upelelezi na Wakuu wa Upelelezi wa mikoa nchini kwa lengo la kupanga mikakati ya kupambana na uhalifu pamoja na kutathmini hali ya uhalifu nchini.

Amesema mtu yeyote amabaye anajihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja kwa kuwa mkono wa Jeshi la Polisi ni mkubwa na kwa wakati huu hakuna upenyo wowote utakaoachwa kwa kuwa operesheni inaendelea nchi nzima.

“Wito wangu kwa wahalifu ni bora watafute kazi nyingine ya kufanya kwa kuwa hatuna huruma kwa watu hao na wananchi waendelee kutupatia taarifa zao ili tuhakikishe nchi yetu inaendelea kuwa salama,” DCI Wambura.

Kwa upande wake Naibu DCI, DCP Faustine Shilogile amesema Idara ya Upelelezi wa makosa ya Jinai Makao Makuu inaendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa takwimu na utoaji wa mafunzo kwa watendaji wa idara hiyo ili kuwa na wapelelezi wenye weledi ambao watasaidia kuharakisha upelelezi wa kesi zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi.

MKE WA TB JOSHUA AFICHUA MWANZO MWISHO ALIVYOFARIKI, ALIOGA, IBADANI, AKAFIA CHUMBA MAALUM

Chanzo: millardayo.com