Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DCEA yawashikilia saba kwa kukutwa na Dawa za kulevya

Drugs 825x510 1 DCEA yawashikilia saba kwa kukutwa na Dawa za kulevya

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: Dar24

Jumla ya watuhumiwa saba, wamekamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), wakiwa na kilo 16. 643 za dawa za kulevya kilo 15.19 za heroin, gram 655. 73 za cocaine na gramu 968.67 za methamphetamine.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya ameyasema hayo ii leo Desemba 7, 2022 na kuongeza kuwa kilo 15.19 za heroine ni za watuhumiwa watatu na wenzake waliokamatwa wakiwa na kilo 34.89 za heroin katika operesheni ya mwanzoni mwa mwezi Novemba 2022.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni ni Suleiman Thabit Ngulangwa (36) mfanyabiashara na mkazi wa salasala, Sharifa Selaman Bakar (41) makazi wa maji matitu, mbagala na Farid Khamis Said (22) mkazi wa maji matitu, Mabagala wote wakiwa ni wakazi wa jijini Dar es Salaam.

Mabadiliko sheria ya Habari kuwasilishwa BungeniMpanda kuadhimisha miaka 61 ya uhuru kwa kupanda mitiKamishna Jenerali Kusaya amesema, watuhumiwa wengine wanne walikamatwa wakiwa na gramu 655.75 za cocaine na gram 968.67 za methamphetamine wakiwa katika harakati za kusafirisha dawa hizo kwenda nje ya nchi ambao ni Hussein Rajab Mtitu (28) anayejulikanapia kama Chodri Mohamed mfanyabiashara na mkazi wa kibonde maji, mbagala.

Wengine ni Jaalina Rajab Chuma (31) anayejulikana pia kama Jaalan Mohan mjasiriamali na makazi wa Tandika, Shaban Abdallah Said (36) mkazi wa Kilimahewa, Tandika, hawa pia ni wakazi wa Dar es Salaam pamoja na Irene Dickson Mseluka (36) mfanyabiashara na makazi wa Ndala Shinyanga, na wote watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Hata hivyo, Kamishna Jenerali Kusaya amesema Mamalaka inashirikiana na makampuni ya usafirishaji wa vifurushi, vyombo vyte vya ulinzi na usalama na wadau wengine katika udhibiti na mapambano dhidi ya dawa za kulevya, ili kukabiliana na mbinu mpya za usafirishaji na uuzaji wa dawa hizo.

Chanzo: Dar24