Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DCEA yatoa onyo wanawake wanaotumiwa kubeba dawa za kulevya

Dawa Za Kulevya Ajisaidia.png DCEA yatoa onyo wanawake wanaotumiwa kubeba dawa za kulevya

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imetoa onyo kwa Wanawake wa kitanzania kuhusu mbinu mpya inayotumiwa na raia wa kigeni ya kusafirisha dawa za kulevya.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imetoa onyo kwa Wanawake wa kitanzania kuhusu mbinu mpya inayotumiwa na raia wa kigeni ya kusafirisha dawa za kulevya. Akitoa onyo hilo leo Jumatatu Juni 19, 2023 Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, Aretas Lyimo amesema kuwa mbinu mojawapo inayotumika zaidi ni raia wa kigeni kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na Wanawake wa kitanzania zaidi ya mmoja na kuwatumia kuficha dawa za kulevya kwenye makazi yao huku wao wakipanga nyumba tofauti na wanapoishi wapenzi wao hali ambayo huwasababishia wanawake hao matatizo baadae.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live