Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DCEA yashinda Kesi tatu za Mapapa wa Dawa za Kulevya

94497419d1f066ffa1f42ddbc8cd307d DCEA yashinda Kesi tatu za Mapapa wa Dawa za Kulevya

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, imesema katika kipindi cha Mwezi Novemba na Desemba 2020, imefafanikiwa kushinda kesi tatu kubwa za wafanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya nchini.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA), James Kaji, amesema kesi hizo zilikuwa zikisikilizwa katika Mahakama ya Uhujumu Uchumi, ambapo DCEA ilishinda baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani Yanga Omari Yanga maarufu ‘Rais wa Tanga’ na kumuhukumu kifungo cha miaka 30 baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine uzito wa gramu 1052.63

Yanga alikamatwa Agosti, 2018 na wenzake wawili mtaa wa Bombo jijini Tanga, wakitaka kusafirisha dawa hizo za kulevya.

Pia mfanyabiashara mwingine aliyetiwa hatiani ni Ayubu Mfaume maarufu ‘Kiboko’ na mkewe Pili Kiboko ambao wamehukumiwa miaka 20 jela kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 251.25.

Kiboko anadaiwa kuwa kiongozi wa ulanguzi wa dawa ya kulevya aina ya heroine amekuwa akifanya operesheni zake kati ya Afrika mashariki na China.

“Kiboko ana vijana 68 ambao wameshikiliwa China, ameharibu maisha ya vijana wengi,” amesema Kaji na kueleza kuwa amekuwa na ushirikiano na walanguzi wa mihadarati nchini Brazil, Pakistani, na Mataifa ya Ulaya.

Pia raia wawili wa Iran nao wametiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa gramu 111.02 katika Bahari ya Hindi na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela pamoja na kutaifishwa kwa jahazi husika.

Chanzo: habarileo.co.tz