Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC amweka mahabusu mkuu wa shule kwa kujihusisha na mapenzi

21197 Dc+pic TanzaniaWeb

Mon, 8 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mkuu wa Wilaya ya Misungwi jijini Mwanza, Juma Sweda amemweka rumande Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Misasi, Deusedent Damas akituhumiwa  kujihusisha na mapenzi shuleni.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Oktoba 5, 2018, Sweda amesema kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati yake, jeshi la polisi, sungusungu na wananchi, waliweza kuweka mtego na kumnasa mwalimu huyo.

Amesema mwalimu huyo kwa sasa ameshikiliwa katika kituo cha polisi Misasi akisubiri uchunguzi ukamilike na hatua nyingine zitafuata.

“Pamoja na kutatua masuala mbalimbali ambayo yanajitokeza kwenye jamii, pia tunahakikisha tunatembelea shule zetu ili kutambua hatua zinazopigwa na ndio tumeweza kumkuta huyu mwalimu,” amesema Sweda.

 

Ofisa Elimu Wilaya ya Misungwi, Diana Kuboja amesema wanalaani kitendo hicho na lazima hatua kali zichukuliwe kwa kuwa jambo hilo ni ukiukwaji wa haki na unyanyasaji.

“Kitendo kama hiki ni fedheha kubwa sana miongoni mwa jamii, hawa ni watoto wadogo ambao hata hatima ya maisha yao hawaitambui,” amesema Diana.

“Mwalimu kushiriki mapenzi na mwanafunzi wake huo ni udhalilishaji wa hali ya juu, sisi kama wadau wa elimu tunalaani kitendo hicho.”

Mmoja kati ya wazazi, Chrisantusi Madoho amesema tabia za walimu kuwadhalilisha wanafunzi ziimekuwa zikiripotiwa lakini ushahidi unapindishwa na kumuomba mkuu huyo wa wilaya kuchukua hatua stahili dhidi ya mtuhumiwa.

Pia, Sweda amesema mwalimu Damas anatuhimwa kufuja Sh30 milioni ambazo zilitolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shuleni hapo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz