Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DAR: 19 Mbaroni akiwemo afisa feki wa serikali

MULIRO 1 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Thu, 20 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watuhumiwa 91 wa uhalifu wa aina mbalimbali ukiwemo wizi wa magari, unyang'anyi wa kutumia nguvu pamoja na kusafirisha na kuuza dawa za kulevya pamoja na watu wanaofanya utapeli kwa kujifanya kuwa ni maofisa wa serikali.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amebainisha hayo leo ofisini kwake ambapo ameeleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika oparesheni maalum uliyofanyika kati ya Januari 1 hadi 12 kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dora.

Kamanda Muliro, amesema katika operesheni hiyo, pikipiki zaidi ya 12 zilizohusishwa na watuhumiwa wa unyanganyi wa kutumia nguvu zimekamatwa, fedha zaidi ya milioni 9 zilizoibwa, pamoja na tapeli sugu anayetumia mwamvuli wa afisa usalama kufanya utapeli kwenye ofisi mbalimbali na kuwa wote waliokamatwa watafikishwa mahakamani ili taratibu za kisheria kuendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live