Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chege afikishwa kortini kwa kujaribu kumuua mama yake

Ethan Chege Ethan Chege

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume ambaye inadaiwa alitishia kumkatakata mamake ameshtakiwa kwa kutishia kuua kinyume na kipengele 223 (1) cha sheria kuhusu uhalifu.

Ethan Chege, 24, alifikishwa katika Mahakama ya Makadara Law Courts na kushtakiwa kwamba alimtishia Anastacia Ndunge ambaye ni mama yake mzazi akiwa nyumbani Ruai, kaunti ndogo ya Njiru jijini Nairobi mnamo Machi 6, 2023.

Mahakama ilielezwa kwamba Chege alimfokea mamake kwa kusema “nitakukatakata kama mboga”. Kwa mujibu wa polisi na upande wa mashtaka, maneno hayo yalikuwa tishio kwa maisha ya mlalamishi.

Chege pia alishtakiwa kwa kuzua vurugu kinyume na kipengele 95 (1) cha sheria kuhusu uhalifu ambapo alimtimua Bi Ndunge kutoka kwa makazi yake.

Vile vile anakabiliwa na shtaka lingine la kuwa na dawa za kulevya kinyume na kipengele cha 3 (1) kuhusu dawa za kulevya baada ya kupatikana akiwa na bangi yenye thamani ya Sh4,900 siku alipokamatwa mnamo Machi 24.

Aidha mahakama iliambiwa mlalamishi alilazimika kutoroka nyumbani na kuenda kwa jirani kabla ya kuripoti na kuandikisha taarifa kwa polisi. Bi Ndunge vile vile alikodisha nyumba tofauti kuepuka hasira za kijana yake.

Hii ni mara ya pili kwa Chege kutishia kumuua mamake. Mwaka 2022 alishtakiwa. Chege alikanusha mashtaka mbele ya Hakimu Mkuu Agnes Mwangi.

Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh200,000. Kesi itatajwa mnamo Aprili 25 kabla ya kusikilizwa mnamo Septemba 20, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live