Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘CUF Lipumba’ wakaidi agizo la Polisi, waendelea na mkutano

46278 Cuf1pic ‘CUF Lipumba’ wakaidi agizo la Polisi, waendelea na mkutano

Tue, 12 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Licha ya Jeshi la Polisi kuzuia mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF)  upande wa Mwenyekiti anayetambulika na ofisi ya msajili wa vyama vya Profesa Ibrahim Lipumba, mkutano huo umeendelea muda mfupi baada ya mwenyekiti hiyo kuwasili ukumbini.

Naibu Katibu mkuu wa chama hicho-Bara, Magdalena Sakaya akizungumza katika mkutano huo leo Jumanne Machi 12, 2019 amesema jumla ya wajumbe waliofika wamefikia 598 hivyo akidi imetimia.

Mkutano huo ambao waandishi wa habari hawaruhusiwi kuingia ukumbini unaendelea ukipata baraka za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, ambapo Naibu Msajili, Sisty Nyahoza ndiye aliyeufungua kwa kutoa hotuba.

Katika hotuba hiyo, Nyahoza amesema mkutano huo unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya CUF ndio maana umetambuliwa na Ofisi yake.

Amewapongeza kwa kile alichosema wamehimili mapito ya mahakama na wameendelea kukilinda chama.

Vilevile amewapongeza kwa kuteua bodi mpya ya wadhamini na kuwakumbusha wajibu wao wa kutunza Mali na fedha.

Amewataka pia kuzingatia mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa.

Nyahoza pia amesema sheria ya sasa ya vyama vya siasa hairuhusu vyama kuwa na vikundi vya ulinzi.

Baada ya hotuba ya Nyahoza, Sakaya ametangaza mchakato wa marekebisho ya CUF.

Licha ya RPC wa Ilala, Zubery Chembera aliyeleta taarifa ya zuio, askari wa jeshi hilo wameendelea kubaki eneo hilo wakiendelea na ulinzi.

Polisi wazuia mkutano wa ‘CUF Lipumba’

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachojiri zaidi



Chanzo: mwananchi.co.tz