Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA waiburuza Polisi Kortini

Chademapic 600x400 CHADEMA waiburuza Polisi Kortini

Mon, 4 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mawakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania wamefungua kesi mahakamani jijini Dodoma kuwalazimisha Polisi kumwachia kwa dhamana mwanachama wao Twaha Mwaipaya.

Wakili Fredrick Kalonga amesema tayari wameshapeleka maombi hayo leo Jumatatu 4 Julai 2022 mahakamani na hadi leo mchana walikuwa wanasubiri kupangiwa Jaji na kupewa namba ya kesi.

Twaha Mwaipaya ambaye ni mratibu wa Uhamasishaji wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) anashikiliwa na Polisi kwa sababu ambazo hazijafahamika.

Mapema leo asubuhi baadhi ya viongozi wa Chadema mkoa na ngazi ya Taifa wamefika kikuo kikuu cha Polisi kwa ajili ya kumwona ambapo wameandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa anaendelea vizuri.

"Ni kweli tumesha file kesi mahakamani, hapa tunasubiri tupangiwe jaji na kupewa namba ya kesi, kwa hiyo sasa hivi hatuwezi kusema zaidi ni hayo," amesema Kalonga.

Awali, Mwaipaya alikamatwa mkoani Morogoro ambako alishikiriwa kwa siku kadhaa hata kusababisha kelele nyingi kwenye mitandao ya kijamii watu wakitaka aachiwe.

Kwenye maombi yao Chadema, mbali na kuwashitaki Polisi, wamemshitaki pia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kwenye maombi yao kikubwa wanaomba Mwaipaya aachiwe kwa dhamana au kesi ipelekwe mahakamani haraka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live