Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bwana harusi, wazazi wa binti wahukumiwa kuandaa harusi ‘haramu’

Jela Mojaaa.png Bwana harusi, wazazi wa binti wahukumiwa kuandaa harusi ‘haramu’

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya imewahukumu wazazi pamoja na aliyekuwa msaidizi wa bwana harusi kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh1,000,000 kwa kosa la kutaka kumuozesha binti (14) ambaye ni mwanafunzi wa darasa sita katika Shule ya Msingi Mkola.

Pia, Mahakama hiyo imemhukumu ‘bwana harusi’ ambaye naye ni mtoto chini ya miaka 18 kifungo cha nje mwaka mmoja na kupewa masharti ya kutotenda kosa baada ya kukiri kutenda kosa hilo.

Akisoma hukumu hiyo Hakika Mkazi wa mahakama hiyo, Paul Ntumo amewataja wazazi hao waliohukumiwa ni Rashid Said (40), mke wake Stomah Sakenke (35), pamoja na aliyekuwa msaidizi wa bwana harusi Sadam Shaban (19) wote wakazi wa Kitongoji cha Ujerumani, Kijiji cha Mkola, Kata ya Mkola mamlaka ya mji mdogo Makongolosi Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Awali, mwendesha Mashtaka Serikali, Mazoya Luchagula akisoma makosa ya ameiambia mahakama washtakiwa walitenda kosa hilo Novemba 10 2021, saa 16:30 katika Kitongoji cha Ujerumani Kata ya Mkola ambapo walikamatwa wakiwa kwenye harusi ya kumuozesha binti huyo.

Baada ya polisi kupewa taarifa kuwa kuna wazazi wanawaozesha walifika eneo la tukio na kuwakamata wakiwa kwenye harusi nyumbani kwao, Bwana harusi ambaye naye alikuwa ni mtoto chini ya miaka 18 na kuweza kuwakamata.

Hakimu Ntumo amesema kosa hilo ni kinyume cha sheria ambapo washtakiwa walikuwa wanne wazazi wa binti, bwana harusi na msaidizi wa bwana harusi walipokamatwa na kufikisha polisi kuchukuliwa maelezo wote walikana.

Baada ya washtakiwa hao kukana kosa, upande wa mashtaka uliweza kufanya upelelezi ili kuthibitisha shauri hilo na kuridhishwa na ushahidi ulioletwa mahakamani hapo.

Awali, Luchagula aliiambia mahakama washtakiwa kitendo walichokifanya ni kibaya ambapo aliomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa jamii yenye tabia kama hizo ili kukomesha vitendo vya ukatili.

Hakika Ntumo amesema anawahukumu wazazi wa binti na msaidizi wa bwana harusi kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada ya kuridhishwa na ushahidi ulitolewa mahakamani hapo ambapo washtakiwa wote watatu walikwenda kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada kushindwa kulipa faini ya Sh 100,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live