Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunduki AK 47 na risasi 176 kwenye makazi ya mkimbizi

5ac47053cd15e06f400eb69a57e138d8 Mkimbizi hatiani kwa uhalifu Kigoma

Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

POLISI mkoani Kigoma wamemkamata mtu aliyetambuliwa kuwa ni raia wa Burundi akituhumiwa kuhusika na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha katika barabara kuu ya Kasulu kwenda Kibondo.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo, James Manyama amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Sabushike Abraham maarufu kwa jina la Kayuki (33).

Mtuhumiwa anadaiwa kuwa ni mkimbizi wa Burundi anayehifadhiwa kwenye kambi ya wakimbizi ya nduta wilayni Kibondo.

Kamanda Manyama alisema mwishoni mwa wiki iliyopita polisi walimkamata mtuhumiwa katika kijiji cha Busunzu wilayani Kibindo akiwa na bunduki aina ya AK 47pamoja na risasi 176.

Alisema mtuhumiwa alikamaatwa baada ya polisi kupata taarifa na wakaweka mtego.

“Baada ya kukamatwa na kuhojiwa aliwapeleka polisi katika kijiji cha Busunzu eneo la Mlimani wilaya ya kibondo mkoani Kigoma ambako amekuwa akificha bunduki yake baada ya matumizi,”Alisema Kamanda Manyama

Chanzo: www.habarileo.co.tz