Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bulaya mgonjwa, ashindwa kuhudhuria mahakamani

49155 Mahakamaniiipic

Thu, 28 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mbunge wa Bunda (Chadema) Ester Bulaya, ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Kisutu, kusikiliza kesi yake kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mgonjwa.

 Bulaya ni mshtakiwa wa tisa katika kesi ya kufanya mikusanyiko isiyo halali inayowakabili vigogo tisa wa Chadema.

 Hayo yameeleza leo Machi 28, 2019 na mdhamini wa Bulaya, Ndeshukurwa Tungaraza wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka.

Ndeshukurwa ambaye ni diwani wa Makongo kwa tiketi ya Chadema, ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba.

“Mheshiwa hakimu, Bulaya ni mgonjwa  amefanyiwa upasuaji Machi 23, 2019 katika Hospitali ya Aga Khan na kuruhusiwa kutoka hospitali hapo Machi 26, 2019, hivyo kutokana na hali yake ameshindwa kufika mahakamani hapa kusikiliza shauri hili,” amedai Tungaraza.

Mdhamini huyo amedai kuwa, Bulaya alilazwa hospitali hapo Machi 22 na Machi 23, mwaka huu ndio alifanyiwa upasuaji.

Related Content

Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kujua kilichojiri katika Mahakama ya Kisutu.



Chanzo: mwananchi.co.tz