Wed, 16 Jun 2021
Chanzo: globalpublishers.co.tz
Breaking News: Viongozi Wa Uamsho Waachiwa Huru June 16, 2021 by Global Publishers
Viongozi wawili kati ya 36 wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed na Mselem Ali Mselem waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi wameachiwa huru.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu leo Juni 16, 2021 amethibitisha kuachiwa kwa viongozi hao na kueleza kuwa amewafutia mashtaka viongozi wote wa jumuiya hiyo na kilichobaki sasa ni taratibu za kutoka gerezani.
Viongozi hao walikuwa mahabusu tangu mwaka 2014 pamoja na wenzao kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya ugaidi ambayo hayana dhamana wameachiwa huru jana Jumanne Juni 15, 2021 baada ya DPP kuwafutia mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.
STORI NA AZIZ HASHIM | GPL
Chanzo: globalpublishers.co.tz