Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Bosi feki’ wa Necta kupanda kizimbani wiki hii

40002 Pic+necta ‘Bosi feki’ wa Necta kupanda kizimbani wiki hii

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Ofisa feki wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) aliyekamatwa Januari 24, 2019 akiendesha ukaguzi katika Shule ya Sekondari Nuru atapandishwa kizimbani siku yoyote wiki hii.

Kwa mujibu wa taarifa za mkuu wa polisi wilaya ya Serengeti, Methew Mgema na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki leo Jumatatu Februari 4, 2019, kwa sasa taratibu zinakamilishwa ili ‘ofisa feki’ huyo apandishwe kizimbani.

Akizungumzia sababu za mtuhumiwa huyo kupelekwa Musoma badala ya alipokamatwa, Ndaki amesema kosa lilianza kutendeka Musoma kisha akaja Serengeti.

“Alianzia mkoani akawapa barua feki kisha wakaenda Serengeti, ndani ya siku mbili hivi atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yatakayokuwa yanamkabili," amesema Ndaki.

Alipoulizwa sababu za mtuhumiwa huyo kutofikishwa mahakamani mapema amesema alianza kuhojiwa na maofisa wa Necta ili kupata taarifa zaidi.

Taarifa zilizolifikia Mwananchi zinaeleza kuwa mtuhumiwa huyo alipopekuliwa alikutwa na vyaraka mbalimbali na alikiri kushirikiana na watu wa kada mbalimbali kufanya utapeli.

Soma zaidi: Bosi ‘feki’ Necta aendesha ukaguzi shuleni, ashtukiwa



Chanzo: mwananchi.co.tz