Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Udart, mkewe na wenzake kuendelea kusota rumande

64032 Pic+kisena

Mon, 24 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Usafirishaji wa Mabasi yaendayo Haraka, maarufu kama Mwendokasi (Udart), Robert Kisena na wenzake, wanaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi wa kesi yao kutokukamilika.

Kisena na wenzake wanne, wakabiliwa na mashtaka 19, yakiwemo ya utakatishaji fedha na kuisababishia UDART hasara ya Sh 2bilioni.

Wakili wa  Serikali, Elizabeth Mkunde ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo Juni 24, 2019, kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Mkunde ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile, wakati shauri hilo lilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

"Upelelezi wa kesi hii bado haujakamilika, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," amedia  wakili Mkunde

Hakimu Rwezile, baada ya kusikiliza maelezo hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 5, 2019 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande.

Pia Soma

Mbali na Kisena, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 38/2019 ni mke wa Kisena, Florence Mashauri; Kulwa Kisena; raia wa China Chen Shi na Mhasibu wa Kampuni hiyo, Charles Selemani Newe.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kati ya Januari Mosi, 2011 na Mei 31,2018 ndani ya jiji la Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu.

 

Katika shtaka la pili, linawakabili washitakiwa wanne ambao ni Kisena, Kulwa, Simon na Florence ambalo ni kujenga kituo cha mafuta ya petroli bila kibali kutoka  EWURA.

Wanadaiwa kutenda  kosa hilo Januari Mosi mwaka 2015 na Desemba 31, 2017 ambapo inadaiwa walijenga kituo hicho eneo la Jangwani bila kibali cha EWURA.

Katika shtaka la tatu washitakiwa hao inadaiwa kwa kipindi hicho wakiwa wakurugenzi walifanya biashara eneo ambalo halijaruhusiwa kujengwa.

Pia katika shitaka la nne inadaiwa waliiba Sh 1.2bilioni  mali ya UDART huku mashtaka manne ni utakatishaji wa fedha.

Mengine ni mashtaka manne ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo; manne ya  wizi; moja kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na moja ni kusababisha hasara UDART.

Chanzo: mwananchi.co.tz