Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi UDART, wenzake wasomewa ushahidi kesi nyingine ya Uhujumu

Bosipiic Data Bosi UDART, wenzake wasomewa ushahidi kesi nyingine ya Uhujumu

Wed, 27 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesoma maelezo ya mashahidi inatarajia kuwaita katika kesi nyingine ya uhujumu uchumi inayomkabili mkurugenzi wa mradi  wa Usafirishaji wa Mabasi yaendayo Haraka, maarufu kama Mwendokasi (UDART), Robert Kisena (miaka 47) na wenzake.

Pia imesema kuwa inatarajia kuwaita mashahidi 30 na kuwasilisha vielelezo 95 vya ushahidi ambavyo ni nyaraka mbalimbali.

Kisena na wenzake wamesomewa ushahidi huo leo Jumatano, Julai 27, 2022, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, mkoa wa Dar es Salaam, ambako kesi ilikuwa imefunguliwa kwa ajili ya uchunguzi wa awali, kabla ya kuhamishiwa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi itakakosilizwa.

Katika kesi hiyo namba 21, iliyokuwa ikisikilizwa na Hakimu Mfawidhi,  Godfrey Isaya washtakiwa wengine ni Charles Newe ( 48) mkurugenzi wa Udart; mfanyabiashara John Samangu ( 66); mtunza fedha wa Udart,  Tumaini Kulwa  ( 44) na mkurugenzi wa kampuni ya Maxcom Africa, maarufu kwa jina la kibiashara la Maxmalipo, Juma Furaji (48).

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 22 ya kuongoza genge la uhalifu, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uwongo, utakatishaji fedha haramu na kuisababishia Udart hasara ya Sh4.5 bilioni.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti Kati ya Juni 2015 na April 30, zote 2016.

Wanadaiwa kuwa walihamisha fedha hizo kutoka katika akaunti ya Udart katika benki ya NMB, tawi la Bank House, kwenda akaunti ya kampuni ya Long Way Engineering Ltd iliyoko Benki ya KCB.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live