Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Takukuru ameshindwa kufikia muafaka wa makubaliano na DPP

90964 Pic+takukuyru Bosi Takukuru ameshindwa kufikia muafaka wa makubaliano na DPP

Mon, 6 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania, Kulthum Mansoor amedai wameshindwa kufikia muafaka wa makubaliano baina yake na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Kulthum anakabiliwa na mashtaka manane, likiwamo la utakatishaji wa fedha kiasi cha Sh1.4 bilioni, katika kesi ya uhujumu uchumi.

Soma zaidi: Upelelezi kesi ya kigogo wa Takukuru unaendelea

Kulthum kupitia wakili wake, Elia Mwingira, ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu Januari 6, 2020 wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Mwingira amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Godfrey Isaya, kuwa waliandika barua ya kukiri na kuomba msamaha kwa DPP, lakini baada ya kuingia kwenye mazungumzo walishindwa kufikia makubaliano.

"Ni kweli tuliandika barua kwenda kwa DPP, kwa ajili ya mazungumzo lakini yalishindikana, hivyo hadi sasa hakuna mwelekeo wowote," amedai Mwingira.

Kulthum Mansooor wa Takukuru amwandikia DPP barua ya kukiri makosa

Mwingira amedai kutokana na kushindwa kufikia makubaliano, waliomba upande wa mashtaka kuhakikisha upelelezi wa kesi hiyo unakamilika kwa wakati.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Isaya, baada ya kusikiliza hoja za pande mbili aliutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi kwa wakati, ili kesi hiyo iweze kuendelea mbele.

Kesi hiyo imeahirishwa, hadi Januari 20, 2020 itakapotajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande.

Kwa mujibu ya hati ya mashtaka inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari 2013 na Mei 2018, mshitakiwa alighushi barua ya ofa ya Agosti 13 mwaka 2003 kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, barua hiyo imetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo huku akijua sio kweli.

VIDEO: Aliyekuwa mkurugenzi Takukuru alala mahabusu, kufikishwa mahakamani leo

Katika mashitaka ya pili, inadaiwa kati ya Januari, 2012 na Mei 2017, Upanga Wilaya ya Ilala, mshitakiwa kwa kudanganya alijipatia Sh5.2.milioni,  kutoka kwa Alex Mavika ambaye ni mfanyakazi wa Takukuru kama malipo ya kiwanja kilichopo Kijiji cha Ukuni Bagamoyo.

Pia, inadaiwa kati ya tarehe hizo, Mansoor alijipatia Sh3 milioni kutoka kwa Wakati Katondo kama malipo ya kiwanja kilichopo maeneo ya Kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Katika mashtaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa kati ya Januari mwaka  2013 na Mei mwaka jana huko maeneo ya Upanga, mshitakiwa alijipatia Sh.1,477,243,000 wakati akijua kuwa fedha hizo ni haramu na ni zao la kosa tangulizi la kughushi.

Chanzo: mwananchi.co.tz