Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi NIDA apata wakili mpya

Kisutu Ed1 Mahakama Kuu Dar es salaam

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: ippmedia.com

MKURUGENZI Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu, amepata wakili wa kumwakilisha baada ya aliyekuwa wakili wake awali, Joseph Ndunguru, kujitoa.

Maimu jana aliifahamisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wakili wake kwa sasa ni Tuli Kaundime wakati kesi hiyo ilipokuwa inatajwa kwa ajili ya kupata taarifa kama amepata wakili.

Agosti 25, mwaka huu, Wakili Joseph Ndunguru aliandika barua ya kujitoa na mahakama ilimpa mshtakiwa muda wa kutafuta wakili mwingine ili kesi iendelee katika hatua ya utetezi.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu, imepanga Septemba 24, washtakiwa waanze kujitetea kwa kuwa tayari mshtakiwa ameshapata mwakilishi.

Upande wa Jamhuri unaongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Zakaria Ndaskoi na upande wa utetezi unawakilishwa na Wakili Tuli Kaundime, James Mwenda na Sosthenes Mbedule.

Maimu anatarajia kuwa na mashahidi si chini ya 20 na vielelezo visivyozidi 10 wakati wa utetezi.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 55 likiwamo la kuongeza genge la uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kugushi kwa lengo la kumdanganya mwajiri, kusababisha hasara, utakatishaji fedha na matumizi mabaya ya madaraka.

Upande wa mashtaka katika kesi hiyo

ulikuwa na jumla ya mashahidi 26 pamoja na vielelezo 45.

Chanzo: ippmedia.com