Kijana maarufu kwa jina la Bonge mkazi wa Mtaa wa Kichangani, Tabata Kinyerezi hajulikani alipo baada ya kuchukuliwa na baadhi ya waendesha bodaboda kwa madai ya kuhusika na wizi wa Pikipiki usiku wa kuamkia Agosti 3, 2023
Inaelezwa Bonge na wenzake walimvamia bodaboda wakati akishusha abiria Kichangani Darajani saa tano usiku, wakamjeruhi na kumtupa mtaroni, ilipobainika Bonge ndiye Mtuhumiwa, akafuatwa nyumbani kwake, inadaiwa akakiri kuhusika kisha kuonesha alipoificha Pikipiki.
Ndipo viongozi wa Serikali ya Mtaa wakamchukua kumhifadhi, muda mfupi baadaye kundi la Bodaboda likavamia na kuondoka naye kusikojulikana.