Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda wawili kizimbani wakituhumiwa kumbaka binti

HUKUMU Bodaboda wawili kizimbani wakituhumiwa kumbaka binti

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Abbasi Mbunda (22), mkazi wa Temeke Sandali na Musa Mohamed (20), mkazi wa Temeke Mikoroshini, wote madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wamefikishwa mahakamani leo Alhamisi Septemba 14,2023 wakikabiliwa na kosa la ubakaji kwa kikundi.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Amadeus Mallya amesema wawili hao walimbaka kwa pamoja binti mwenye umri chini ya miaka 18 huko maeneo ya Temeke Sandali.

"Mnamo Mei 25, 2023 watuhumiwa kwa pamoja walifanya mapenzi na mwathiriwa bila ridhaa yake kinyume na kifungu 130 (1), (2) (e) na 131A (1), (2) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu namba 16 marejeo ya mwaka 2022," amesema.

Mbali na shtaka hilo, mtuhumiwa namba 1, Abbasi Mbunda anakabiliwa na shtaka lingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile na binti huyo.

Inadaiwa kuwa Mei 25, 2023 mtuhumiwa alimbaka kinyume na maumbile binti huyo mwenye umri chini ya miaka 18 kinyume na kifungu cha 154 (1) (a) na (2) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu namba 16 marejeo ya mwaka 2022.

Wawili hao wamekana kuhusika na makosa hayo na Hakimu Mkuu Mkazi, Ajali Milanzi ameahirisha shauri hilo mpaka Oktoba 5, 2023 litakaposikilizwa tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live