Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti wa miaka 13 auawa na kaka yake, Morogoro

Mauaji Mtoto Moro Tukio hilo limetokea jana mkoani Morogoro

Wed, 16 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto mwenye umri wa miaka 13 anayejulikana kwa jina la Faidhati Ibrahim ameuawa na kaka yake kwa kukatwa na panga sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo shingoni na kichwani.

Tukio hilo limetokea Jana Februari 15, 2022 majira ya saa 11 jioni katika mtaa wa Tambuka reli kata ya Kingolwila Manispaa ya Morogoro ambapo mtuhumiwa alifika katika nyumba ya familia hiyo na baada ya kumkuta mtoto huyo akiwa peke yake alianza kutekeleza unyama huo.

Faidhati Ibrahim alikuwa mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Mwenge iliyopo kata ya Kingolwila Manispaa ya Morogoro.

Kwa Upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Juma Muitano amekiri kutokea kwa tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live