Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti miaka 8 abakwa, mtuhumiwa anadunda mtaani

Mtoto Aliyebakwa Binti miaka 8 abakwa, mtuhumiwa anadunda mtaani

Tue, 30 Aug 2022 Chanzo: EATV

Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Sunday (46), mkazi wa mtaa wa Mkudi, Kata ya Nyamanoro Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza, anadaiwa kumbaka mtoto wa 8 (Pichani) na kumsababishia maumivu makali ikiwemo kumharibu kisaikolojia.

Mtoto huyo akizungumzia tukio hilo amesema mwanaume huyo alimuita wakati akiwa anacheza na kumvutia ndani.

"Nilikuwa nacheza ndipo Sunday akaniita akanivuta ndani akaniambia naomba nikubake nikakataa, nilivyokataa nikataka kupiga kelele akaniziba mdomo akanitishia kisu, akanivua nguo akanibaka kisha akanipa shilingi mia tano akamaliza akafunga mlango akaondoka baada ya mama kujua nimebakwa akamuita bibi ndipo tukaenda polisi", ameeleza mtoto huyo

Wakizungumza kwa uchungu wazazi wa mtoto huyo wameviomba vyombo vya dola kuwasaidia kutokana na mtoto wao kuharibiwa na kupata maumivu makali huku akitakiwa kutumia dawa mwezi mzima ili kumuepusha na maambukizi ya virusi vya Ukimwi lakini wanashangaa mtuhumiwa akiwa nje kwa dhamana licha ya kumfungulia kesi ya ubakaji na ushahidi kuwepo.

Chanzo: EATV