Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti miaka 18 adaiwa kutoa mimba ‘guest’

99721 Pic+bint Binti miaka 18 adaiwa kutoa mimba ‘guest’

Fri, 20 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Polisi Mkoa wa Morogoro nchini Tanzania inamshikilia Rehema Fabiani (18), mfanyakazi wa Mgahawa wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) akidaiwa kutoa mimba akiwa katika nyumba ya kulala wageni ya EM mjini Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Machi 20, 2020 Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema binti huyo alikutwa katika nyumba hiyo akiwa tayari katoa mimba na kusababisha kifo cha kichanga chenye jinsi ya kiume.

Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea jana Alhamisi Machi 19, 2020 saa 3 asubuhi katika nyumba hiyo ya kulala wageni eneo la mtaa wa Amani kata ya Mjimkuu.

Amesema binti huyo alifika katika nyumba hilo na kupanga chumba namba saba na siku iliyofuata asubuhi muhudumu wa nyumba hiyo alisikia kelele kutoka ndani ya chumba hicho na kumgongea.

Kamanda huyo anasema baada ya kufungua mlango wa chumba na kuingia ndani alimkuta binti huyo akilalamika maumivu makali ya tumbo na kumuhoji ambapo alimweleza alikuwa ametumia dawa za kutibu ugonjwa wa UTI.

Amesema baada ya kuhojiwa kwa kina binti huyo alisema aliingia katika nyumba hiyo ya kulala wageni tangu Machi 15, 2020 akiwa na lengo la kuharibu ujauzito aliokuwa nao na alieleza alitumia dawa za aina mbalimbali bila mafanikio na kwamba ndipo Machi 18, 2020 akabadilishiwa dawa na kutimiza lengo lake.

Pia Soma

Advertisement
Akizungumza na mwandishi wa Mwananchi muhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni Ashura Juma amesema, binti alifika akihitaji chumba kama walivyo wateja wengine ambapo alimpokea na kusaini katika daftari la wateja.

Naye Mwenyekiti wa mtaa wa Amani Ramadhani Manyanga amesema majira ya saa 1.30 asubuhi aliitwa na mmiliki wa nyumba ya wageni, Elizabert Mapunda kwa kumpigia simu kuwa kuna mteja wake amepanga hapo kuwa hajamlipa fedha yake lakini mbali na hivyo kuna tukio la kusikitisha lililofanywa na binti huyo.

“Nikiwa mlinzi wa amani katika mtaa wangu nilifika na kukuta binti huyo akiwa tayari kaharibu mimba na kuingia katika chumba nikakuta kitoto kimetoka na binti akawa analia kwa machungu kila nikimuhoji alisema yeye anatokea Mlali alishindwa kuendelea kunieleza,” amesema.

Alisema kutokana na tukio hilo, mwenyekiti huyo aliamua kwenda kutoa taarifa polisi.

Chanzo: mwananchi.co.tz