Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti kidato cha pili auwawa kwa kosa la kuiba kuni

2ef3b7d739f3252e743a7e51a191000c Binti kidato cha pili auwawa kwa kosa la kuiba kuni

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia Said Shabani (39) kwa kosa la kumuua Naomi James (17) mwanafunzi wa kidato cha pili, Shule ya Sekondari Kivukoni, mkazi wa Mtaa wa Nyatorotoro B, Kata ya Nyankumbu wilayani Geita Mkoani Geita kwa kumutuhumu kuiba kuni.

Akizungumza tukio hilo leo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa (RPC) Henry Mwaibambe alisema tukio hilo lilitokea januari 18 mwaka huu katika msitu wa shamba la miti lililopo kata ya Nyankumbu ambapo marehemu alikuwa na wenzake wawili wakiwa wanatafuta kuni.

RPC Mwaibambe alisema wakati marehemu na wenzake wakiendelea kazi hiyo kwenye shamba linalomilikiwa na Said Shabani, ndipo mmiliki huyo alianza kuwakimbiza na bahati mbaya marehemu alianguka chini na kuazan kushambuliwa na mtuhumiwa kwa kitu chenye ncha kali na kusababisha kifo chake.

Katika tukio jingine Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia Mpali Juma (24) mkazi wa kitongoji cha Chokonoka, kijiji cha Bukagu kata ya Kharumwa tarafa ya Msalala wilayani Nyanghwale mkoani hapa kwa kosa la kumuua mke wake aitwaye Esther Mashaka (30).

RPC Mwaibambe alisema mtuhumiwa huyo alitenda tukio hilo januari 16 mwaka huu kwa kumkata na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili na kuutelekeza mwili polini.

Alisema chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa kifamilia uliopelekea wawili hao kutengana kiasi cha kumfanya mtuhumiwa huyo kwenda kwao na marehemu kudai arudishiwe mahali kiasi cha Sh.Laki nne alizotoa wakati anamuoa.

"Marehemu alimujibu kuwa mahali hana kwa muda huo, waende kwa kaka yake akampatie, ndipo njiani alitekeleza mauaji hayo, tumeshamkamata na tutamufikisha mahakamani upelelezi utakapokamilika," alisema RPC.

Aidha RPC Mwaibambe alithibitisha kutokea kwa tukio la kifo cha Kulwa Zacharia mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, Shule ya Sekondari Businde baada ya kujinyonga kwa kutumia mtandio kutokana na kutokubalina na baba yake shule aliyowahamishia yeye na pacha wake.

"Chanzo cha tukio hili ni marehemu na pacha wake walikuwa wamefaulu kwenda shule ya kutwa Businde, lakini baba yao alikuwa anafanya mpango waende shule ya Bweni Ushirombo, mapacha hao hawakuipenda shule hiyo, walitaka waende shule ya mbali, mzazi wao hakukubaliana nao, ndipo marehemu akachukua maamuzi hayo," alisema RPC.

Chanzo: habarileo.co.tz