Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti auawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana

Binti Auawa Binti auawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana

Sat, 5 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Kibosho Kirima katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili.

Mary Mushi anayekadiriwa kuwa na miaka 30 aliuwawa kisha mwili wake kutupwa kwenye shamba la nyumbani kwao.

Mauaji haya ya kutisha yamefanyika usiku na watu waliotekeleza mauaji hayo walifika nyumbani kwa marehemu na kumpigia simu majira ya saa tatu usiku kisha kuondoke naye na kufanya unyama huo na Mwili wake uliokotwa kesho yake katika shamba la nyumbani kwao .

Uongozi wa serikali ya Kijiji unasema umetoa taarifa kwa jeshi la polisi na tayari uchunguzi umeanza.

Mwili wa marehemu umechukuliwa na makachero wa polisi kwa uchunguzi na utahifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kueleza kuwa, wanamshikilia mtu mmoja, na kwamba uchunguzi unaendelea ili kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo.

Kamanda amesema taarifa za awali zinaonyesha kuwa tukio hilo limesababishwa na wivu mapenzi na kwamba uchunguzi bado unaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live