Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti amuua Mama yake na kumng’oa macho (+Audio)

Screenshot 2021 07 08 At 11.18.21 660x400.png Binti amuua Mama yake na kumng’oa macho (+Audio)

Thu, 8 Jul 2021 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Said Mtanda amesema kuwa binti wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Kindi iliyopo wilayani humo anatuhumiwa kufanya mauaji ya mama yake mzazi kwa kumnyonga kwa kutumia shuka na kisha kumpiga na kitu kizito kichwani.

Taarifa hiyo imekuja baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuzungumza na vyombo vya habari na kudai kuwa tukio hilo limetokea Julai 5, 2021 katika eneo la Kibosho Sambarai baada ya binti huyo kutofautiana na Mzazi wake huyo.

Imeelezwa kuwa mama huyo ajulikanaye kwa jina la Marietha Mushi baada ya kuuawa pia aling’olewa macho na binti yake huyo ambaye yupo mikononi mwa Polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi.

Chanzo: millardayo.com