Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bidhaa zanaswa tuhuma ya kodi

56946 Pic+bidhaa

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kibaha.Basi kampuni moja (jina linahifadhiwa kwa sasa) limekamatwa na jeshi la polisi mkoani Pwani likiwa na shehena ya bidhaa za dukani ikiwamo nguo na mafuta ya kupikia zenye thamani ya mamilioni ya shilingi zinazodaiwa kuwa hazijalipiwa kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa alisema basi hilo lililokuwa likitokea Mombasa nchini Kenya lilikuwa na abiria tisa pamoja na shehena ya mizigo hiyo.

“Tulipata taarifa kutoka kwa wananchi wazalendo ambao ni wasiri wetu juu ya basi hilo na tukaweka mtego na hatimaye tukalikamata asubuhi kwenye stendi ya mabasi hapa MailiMoja Kibaha na tulipolipekuwa tumekuta shehena hiyo ambayo tuna amini huenda mzigo huu haujalipiwa ushuru wa Serikali,” alisema

Alisema pamoja na suala la kodi, lakini pia kwa mujibu wa sheria basi la abiria haliruhusiwi kupakia mzigo mkubwa kupita kiasi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na kanuni za usagirishaji abiria.

Meneja wa TRA mkoa wa Pwani, Euvensia Lwiwa alisema amewasiliana na timu ya kudhibiti magendo kutoka makao makuu ya mamlaka hiyo ili wafike eneo la tukio kufanya ukaguzi wa kina na endapo watabaini uwapo wa ukiukwaji wa sheria hatua za kisheria zitachuliwa dhidi ya wahusika.

Kwa upande wake, mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Pwani, Mossi Ndozero aliwataka abiria kujenga tabia ya kutoa taarifa polisi wanapoona magari ya abiria yamesheheni mizigo kupitia kiasi ili hatua zichukuliwe kudhibiti ajali.

Pia Soma

Mmoja wa abiria waliokuwa wanasafiri na basi hilo Zuhura Athumani alisema kuwa alipanda basi hilo mkoani Tanga na kwamba hakutambua kuwa ndani yake kuna shehena ya mzigo mkubwa kiasi hicho.

Jitihada za kuwapata wamiliki wa basi hilo pamoja na shehena hiyo ya mizigo hazikufanikiwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz