Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bibi wa miaka 80 asimulia anavyocharazwa viboko na mwanaye

67036 Bibipic

Tue, 16 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kenya. Lydia Wangechi (80), ameieleza mahakama nchini Kenya jinsi mwanaye,  William Gacheru alivyokuwa akimcharaza viboko bila huruma.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 16, 2019  wakati akitoa ushahidi wake katika Mahakama ya Karatina iliyopo Kaunti ya Nyeri, Kenya.

Wangechi amefungua kesi katika mahakama hiyo akidai mwanawe wa kumzaa amekuwa akimpiga na kumjeruhi.

Kwa mujibu wa ushahidi huo, Wangechi amedai Gacheru alikuwa akimtukana  na kumpiga bila huruma tangu mumewe alipofariki dunia.

Mbele ya Hakimu Mkuu wa Karatina, Alice Mwangi, bibi huyo amedai Februai 6, 20q8 mtoto huyo alimpiga kichwani na kupata jeraha kubwa na kupelekwa Hospitali ya Karatina level 4 kwa ajili ya matibabu.

Huku akitoa ushahidi akiwa analia na kusababisha waliokuwepo mahakamani hapo wengi kuangua vilio, ameieleza mahakama kitendo hicho kimemuuma kwani hata mumewe ambaye waliishi katika ndoa kwa miaka mingi hakuwahi kumpiga.

Pia Soma

“Baada ya mume wangu kufariki dunia mtoto ambaye nimemzaa mwenyewe amekuwa akinipiga sana. Nimejaribu kujizuia kumshtaki nikidhani atarekebika lakini hilo halijafanyika. Sasa nahisi nimefika mwisho,” amedai.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz