Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bibi wa miaka 70 atupwa jela miaka 8 kwa mauaji ya mwanae

E500cf51 D9f6 4f1e 9dc2 765be4c12fd4 Bibi wa miaka 70 atupwa jela miaka 8 kwa mauaji ya mwanae

Sat, 17 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro imemuhukumu Monica Mgaza(70) kutumikia kifungo cha miaka nane gerezani kwa kosa la kula njama na kumuua bila kukusudia Samweli Ngilwa ambaye ni Mtoto wake ili aweze kurithi nyumba.

Akisoma hukumu hiyo ya shauri namba 32 ya mwaka 2020 Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Masseka Chaba amesema February 27 mwaka 2017 Monika pamoja na wezake wawili Abdalah Idd na Rajabu Omary ambao wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela, wanadaiwa kutenda kosa hilo kisha kumtupa Marehemu katika mashamba ya Mkonge Kijiji cha Rudewa Wilayani Kilosa.

Jaji Chaba amesema Washtakiwa wamekiri kutenda kosa hilo mbele ya Mahakama ambapo Mahakama kwa kuangalia afya na umri wa Watuhumiwa imewapa adhabu hiyo ili iwe fundisho.

Aidha Jaji Chaba amesema Mahakama hiyo sio mwisho wa chombo cha kutoa haki na Washitakiwa wana haki ya kukata rufaa endapo hawajaridhika na hukumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live