Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bibi wa miaka 60, amuua mumewe kisa kumtaka azae

Jenezaa K.jpeg Bibi wa miaka 60, amuua mumewe kisa kumtaka azae

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nanlongo Babirye kutoka Uganda amekamatwa kwa kumuua mume wake kufuatia shinikizo za marehemu kumtaka amzalie mtoto.

Akiwa na umri wa miaka 50, Richard Ssemambo alikuwa akitamani mtoto na alimsukuma sana mke wake wa miaka 60, kumzalia.

Pulse Uganda ilimnukuu msemaji wa polisi Fred Enanga, akisema wanandoa hao walitofautiana kuhusu suala hilo usiku wa kuamkia Jumamosi, Machi 4, 2023, katika mji wa Kasangati.

"Wanandoa hao walikuwa wameenda eneo la Kasangati walipotofautiana kuhusu kupata mtoto. Wanandoa hao walipofika nyumbani, mke alichukua mkuki na kumchoma mumewe. Nnalongo alimfunga tu kipande cha kitambaa mumewe jambo ambalo halikusaidia kwa sababu alivuja damu usiku kucha. Ssemambo alikutwa amekufa siku iliyofuata.”

Enanga pia alifichua kwamba kulikuwa na madai kuwa Ssemambo aliwaua watoto wa Nanalongo (watoto wake wa kambo) alipokuwa akiitisha watoto kutoka kwake.

Nnalongo ameshtakiwa kwa mauaji na alikamatwa pamoja na majirani zake wanne. Wanne hao walikuwa wapangaji wa Nnalongo na walikamatwa wakituhumiwa kusaidia katika mauaji.

"Tulikamata watu wengine wanne pamoja naye. Walitazama tu uhalifu ukiendelea kumaanisha kwamba walisaidia uhalifu,” Enanga alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live