Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bibi kizee wa miaka 100 auawa ugomvi wa ardhi

Newslite1641896977825 Bibi kizee wa miaka 100 auawa ugomvi wa ardhi

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: Mwananchi

Bibi kizee wa miaka 100, mkazi wa Kijiji cha Kirongo Juu, Kata ya Kirongo Samanga, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Felister Epiphan Silayo ameuawa na mwali wake kwa kumpiga na kitu kizito kichwani (kisogoni) akipigania ardhi yake kwa zaidi ya miaka 10.

Inadaiwa kuwa, bibi huyo wakati anaingiza majani ya mbuzi ndani akiwa mlangoni mwanamke huyo alimvamia kwa nyuma na kumpiga na kitu kizito kichwani  hali ambayo ilipelekea kuanguka chini na kuvuja damu nyingi.

Kwa taarifa iliyotolea na mmoja wa familia inadai kuwa, bibi huyo ambaye alikuwa ni mjane alikuwa na watoto wawili, wakike na wa kiume ambapo aligawa shamba lake mara mbili.

Baada ya kugawa shamba hilo, mume wake na mtuhumiwa alipewa eneo lake pamoja na dada yake ambapo baada ya mgawo huo, mwali wake huyo aligoma kuondoka nyumbani anakoishi bibi huyo aking'ang'ania kuchukua maeneo yote mawili jambo ambalo lilizua mgogoro wa muda mrefu na kusababisha hata mwanaye wa kiume kutoroka.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  Agosti 13, mwaka huu nyumbani kwa bibi huyo ambapo chanzo cha mauaji ni mgogoro wa ardhi.

"Huyu bibi alipigwa na kitu kizito kichwani upande wa nyuma (kisogoni) na kufariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Huruma na chanzo cha mauaji haya ni mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu tangu mwaka 1990," amesema.

Kamanda Maigwa amesema mauaji ya bibi huyo yalifanywa na mwali wake anayeshikiliwa kwa sasa pamoja na hawara yake ambapo baada ya kufanya mauaji hayo alitokomea kusikojulikana na kwamba Jeshi la Polisi linamsaka mwanaume huyo.

Chanzo: Mwananchi