Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bavicha wahoji alipo mwanafunzi wa Udom

92947 Pic+bavicha Bavicha wahoji alipo mwanafunzi wa Udom

Fri, 24 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limeuomba uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom)  na polisi kueleza alipo mwanafunzi wa chuo hicho, Mugaya Tungu.

Taarifa zilianza kusambaa kwenye  mitandao ya kijamii kuanzia Januari 22, 2020 zikieleza kuwa mwanafunzi huyo wa mwaka wa pili anayesoma sayansi asili, alikamatwa na polisi Januari 21, 2020 akidhaniwa kuwa ndiye aliyepiga picha za wanafunzi wa Udom wakiwa katika foleni ndefu wakiwa na madumu ya maji.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwanafunzi huyo alikamatwa akiwa chumbani kwake na kupelekwa kituo cha polisi Chimwaga lakini wanafunzi wenzake walipomfuatilia kituoni hapo  walimkosa na kuambiwa  amedhaminiwa  ingawa haonekani chuoni na simu zake hazipatikani.

Hata hivyo Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alilieleza Mwananchi kuwa hana taarifa za polisi kumkamata mwanafunzi huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Januari 24, 2020 makamu mwenyekiti wa Bavicha, Moza Mushi amesema kuna jambo linajificha, kutaka chuo na polisi kueleza ukweli.

"Tunalaani kitendo cha uongozi wa chuo na polisi Mkoa wa Dodoma kutoeleza ukweli alipo mwanafunzi huyu kwani baada ya kukamatwa na kupelekwa polisi Chimwaga alifuatiliwa na taarifa iliyotolewa kituoni hapo ni kwamba ameshadhaminiwa na mtu ambaye hawakumtaja jina.”

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
“Tangu alipodhaminiwa kituoni hapo  haonekani wala haujulikani alipo na simu zake  hazipatikani polisi waeleze ni nani aliyemdhamini,” amesema Moza.

Katibu wa serikali ya wanafunzi Udom, Paschal Michael amekaririwa akisema hana taarifa yoyote kuhusu mwanafunzi huyo, amekiri kumfahamu.

Chanzo: mwananchi.co.tz