Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bastola ya Nape yakamatwa Mbeya

Thumb Bastola Yapatikana N5cdd071927015 660x400 Bastola ya Nape yakamatwa Mbeya

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Mbeya, limefanikisha kuipata bastola ya mbunge wa jimbo la Mtama Nape Nnauye, iliyoibiwa nyumbani kwake maeneo ya Kawe.

Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 18, 2021, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa, na kusema kuwa bastola hiyo iliibiwa Februari 15, 2021, majira ya saa 11:00 alfajiri nyumbani kwake maeneo ya Kawe.

Aidha SACP Mambosasa ameongeza kuwa bastola hiyo aina ya GLOCK 17 yenye No. YX647 ikiwa na risasi 14 ndani ya kasha lake, imekamatwa jana mkoani Mbeya na mtuhumiwa wa wizi wa silaha hiyo anashikiliwa na jeshi la polisi.

MTANZANIA AUNDA MAGARI, CROWN ATHLETE IPO, ANAPIGA HELA “WAZUNGU WANANUNUA”

Chanzo: millardayo.com