Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Basi lililobeba wanafunzi lakamatwa na mirungi

Mirungi Pic Basi lililobeba wanafunzi lakamatwa na mirungi

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, linawashikilia wafanyakazi watatu wa basi la kampuni ya Extra Luxury kwa kukutwa na bunda 316 na kilo 55 za mirungi zilizokuwa ndani ya gari hilo lililobeba wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha Science waliokuwa wanakwenda likizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatatu Desemba 11, 2023, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjqro, Simon Maigwa amesema gari hilo lilikamatwa Desemba 6, mwaka huu, saa nne na nusu asubuhi, katika eneo la majengo mapya, Hedaru, Wilaya ya Same likitokea mkoani Arusha kwenda Dar es Salaam.

Kamanda Maigwa amesema baada ya polisi waliokuwa doria kupata taarifa za gari hilo kuwa limebeba dawa hizo za kulevya lilipofika eneo la Majengo, wilayani Same walifanya upekuzi ndani ya gari hilo na kwenye buti walikuta dawa hizo za kulevya.

Kamanda Maigwa amesema watuhumiwa hao watatu ambao ni wafanyakazi wa kampuni hiyo, watafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live