Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bangi, gongo, samaki wachanga vyawaingiza matatani watu 18

10385 Pic+bangi TanzaniaWeb

Mon, 6 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Polisi mkoani Mwanza inawashikilia watu 18 kwa tuhuma za kukutwa na samaki wachanga kilo 125 wilayani Sengerema.

Taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi mwishoni mwa wiki iliyopita inasema watu hao pia walikamatwa wakiwa na nyavu haramu 50 za kuvulia samaki aina ya timba na kilo mbili za bangi.

Kamanda Msangi alisema watuhumiwa walikamatwa katika operesheni iliyofanyika Agosti 2 na 3 katika maeneo kadhaa ndani ya Ziwa Victoria.

Kamanda Msangi alisema kuwa watuhumiwa pia walipatikana na gongo lita 265, pikipiki inayodaiwa ni ya wizi na nyavu haramu 600.

Alisema polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa katika maeneo ya vijiji vya pembezoni mwa Ziwa Victoria na kwenye visiwa vya wilayani Sengerema wapo watu wanaojihusisha na biashara haramu ya gongo na dawa za kulevya. (Ngollo John)

Chanzo: mwananchi.co.tz