Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu wa miaka 89 mbaroni kwa kumbaka mjukuu wake

MWAIBAMBE WEB.jpeg Kamanda Mwaibambe

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JESHI la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mzee aitwaye, Grevas Katemi (89) mkazi wa Nyamisebeyi, wilayani Biharamulo mkoani Kagera kwa tuhuma za kumwingilia kimwili kinguvu mjukuu wake wa miaka 20.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa, Henry Mwaibambe ameelezea tukio hilo wakati akiwasilisha taarifa ya matukio yaliyojitokeza na kuvuta hisia kwa jamii kwa kipindi cha mwezi Juni 2021 hadi Februari mwaka huu.

Amesema mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Februari 6 mwaka huu, majira ya saa nane usiku ambapo alimwingili kimwili mjukuu wake aitwaye Grace Tano akiwa amelala.

“Ni kwamba mnamo Februari tano 2022, Modesta Katemi (54) mkazi wa mtaa wa Magogo (mjini Geita alipigiwa simu) na baba yake mzazi (Grevas Katemi) akimtaka amutumie wajukuu zake wakamsaidie kazi za kwenye mgahawa.

“Ndipo wajukuu wawili ambao ni Grace Tano (20) na mdogo wake Elizabeth Tano waliruhusiwa na kuweza kufika siku hiyo hiyo hadi nyumbani kwa babu yao huko Biharamulo,” ameeleza.

Ameongeza “Ilipofika majira ya saa nane usiku babu huyo alimfuata mjukuu wake Grace, mahali alipokuwa amelala na kuweza kumwingilia kimwili yaani kubaka,”.

Ameeleza baada ya kutenda tukio hilo Mzee Katemi (Babu) alikataa wajukuu zake kutorudi kwa wazazi wao huku akiwataka kutotoa taarifa za tukio hilo kwa wazazi wao na endapo watasema basi lazima watakufa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live