Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba na marafiki zake wakamatwa wakipanga kumuozesha Binti wa miaka 14

Images 4.jpeg Baba na marafiki zake wakamatwa wakipanga kumuozesha Binti wa miaka 14

Fri, 4 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Watu watano akiwamo baba mzazi wakazi wa Kijiji cha Mwawile, wilayani Misungwi mkoani Mwanza, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kula njama za kutaka kumuoza binti wa miaka 14 kwa mahari ya ng’ombe tisa na fedha taslimu Sh. 100.000.

Binti huyo alitaka kuozwa kwa mwanamume mwenye miaka 40, Buholo Lukuyege.

Sakata hilo lilitokea juzi, baada ya muuguzi wa zahanati ya Mwawile kutoa taarifa kwa mamlaka husika kufuatia wachumba hao kufika kwake kwa ajili ya kupima afya zao.

Akizungumzia tukio hilo, mjomba wa binti huyo, Juma Lukuyege, alisema mtoto huyo hakufanikiwa kumaliza elimu ya msingi na aliishia darasa la kwanza.

WAZIRI MKUU KUFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI SADC “TUNAWEZA UZA HATA DOLA BILIONI 2”

Chanzo: millardayo.com