Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba mzazi mbaroni kwa tuhuma mauaji ya mwanae

56955 Pic+mauaji

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Polisi mkoa wa Mbeya  linamshikilia baba mzazi wa marehemu Rose Japhet (6), mkazi wa Msewe kata ya Igurusi-Mbarali, mkoani humo na mfanyabiashara mmoja kwa tuhuma za kuhusika kwa mauaji ya mtoto huyo ili  kujipatia utajiri.

Taarifa iliyotolewa jana Jumamosi Mei 11 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei ilisema watu wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya mtoto huyo ni baba mzazi wa mtoto huyo na mfanyabiashara anayemiliki shule ya sekondari wilaya ya Mbeya.

Kamanda Matei alisema Mei 3 muda wa saa 3:00 usiku katika eneo la msitu wa Hifadhi wa Chimala-Mbarali, mtoto huyo alikutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo kisha kukatwa kanyagio la mguu wake.

Alisema katika msako wa polisi, kanyagio la mtoto huyo lilikutwa limefukiwa eneo la Mbalizi wilaya ya Mbeya.

"Chanzo cha tukio hili ni tamaa ya kupata utajiri. Baba mzazi wa marehemu mtoto huyo alimtoa mwanae huyo kwa mfanyabiashara huyo (mtuhumiwa wa pili) ambaye ni mmiliki wa shule ya sekondari kwa malipo ya Sh5 milioni,” alisema.

Lengo auawe na kisha kanyagio la mguu wa kulia na kupatiwa mfanyabiashara huyo na apeleke kwa mganga ili amtengenezee dawa ya utajiri  aweze kufanikiwa kwenye biashaara zake za shule anayomiliki," alisema Kamanda Matei.

Habari zinazohusiana na hii

Kamanda Matei alisema mfanyabiashara huyo baada ya kuhojiwa alikiri kuhusika na tukio hilo na wanaendelea na uchunguzi wa kina pamoja na kumtafuta mganga aliyetarajiwa kupelekewa kiungo hicho (kanyagio) kwa hatua zaidi za kisheria.

Chanzo: mwananchi.co.tz