Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba mzazi apandishwa kizimbani akituhumiwa kuwakeketa mabinti zake

90991 Pic+keketa Baba mzazi apandishwa kizimbani akituhumiwa kuwakeketa mabinti zake

Tue, 7 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar ss Salaam. Baba wa watoto watatu, Cosmas Chacha (45) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka matatu ya kuwakeketa watoto wake hao na kuwasababishia maumivu makali sehemu zao za siri.

Chacha ambaye ni mkazi wa Kivule jijini Dar es Salaam amefikishwa Mahakamani hapo leo Jumatatu Januari 6, 2020 na kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rashidi Chaungu.

Akisoma mashitaka hayo, Wakili wa Serikali, Faraji Nguka amedai Desemba 8, 2019  katika eneo la Kivule Dar es Salaam, mtuhumiwa huyo akiwa baba mzazi na mwenye jukumu la kuwalea watoto wake watatu aliwapeleka kufanyiwa ukeketaji hali iliyowasababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo, upande wa mashtaka ulidai uchunguzi wa kesi hiyo bado unaendelea hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Chaungu akitoa masharti ya dhamana alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili wenye barua na vitambulisho na barua zinazotambulika pamoja na kusai bondi ya Sh5 milioni.

Hata hivyo mshtakiwa huyo ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana na kupelekwa rumande, kesi hiyo itatajwa tena Januari 20, 2020.

Chanzo: mwananchi.co.tz