Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba mzazi adaiwa kuua mwanaye kwa malipo ya Sh5 milioni

56874 RPC+Mbeya

Mon, 13 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Baba mzazi wa marehemu mtoto Rose Japhet(6), mkazi wa Msewe kata ya Igurusi-Mbarali, mkoani Mbeya, na mfanyabiashara mmoja wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika kwa mauaji ya mtoto  huyo  ili  kujipatia utajiri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei alisema watu wanaotuhumiwa na kuhusika na mauaji ya mtoto huyo ni baba mzazi aliye lipwa Sh5 millioni na mfanyabiashara anayemiliki Shule ya sekondari iliyopo Mbalizi, Wilaya ya Mbeya.

 

Kamanda Matei alisema, Mei 3, mwaka huu, muda wa saa 3 usiku katika eneo la msitu wa Hifadhi wa Chimala-Mbarali, marehemu mtoto huyo alikutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo kisha kukatwa kanyagio la mguu wake.

 

Alisema katika msako wa Polisi, kanyagio la mtoto huyo lilikutwa limefukiwa eneo la Mbalizi wilaya ya Mbeya.

Pia Soma

 

"Chanzo cha tukio hili ni tamaa ya kupata utajiri. Baba mzazi wa marehemu mtoto huyo alimtoa mwanae huyo kwa mmiliki wa shule kwa malipo ya Sh5 milioni.”

 

“Lengo auawe na kisha kanyagio la mguu wa kulia kupatiwa mfanyabiashara huyo na apeleke kwa mganga ili amtengenezee dawa ya utajiri (ndagu) aweze kufanikiwa kwenye biashaara zake za shule anayomiliki," alisema Kamanda Matei katika taarifa ya polisi leo, Mei 11, 2019.

 

Kamanda Matei alisema, mfanyabiashara huyo baada ya kuhojiwa alikiri kuhusika na tukio na wanaendelea na uchunguzi wa kiina pamoja na kumtafuta mganga aliyetarajiwa kupelekewa kiungo hicho kwa hatua zaidi za kisheria.

Chanzo: mwananchi.co.tz