Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba, mama mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wao

Crime Scene 45.jpeg Baba, mama mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wao

Thu, 31 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paskari Erinest(46) na mkewe Jeska Balitazali (39) wote wakazi wa Sengerema wanashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wao Aneth John(8) mwanafunzi wa darasa la awali Shule ya Msingi Nyancheche wilayani Sengerema.

Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Hamis Mwampelwa amedai moto huyo amepoteza maisha Machi 29, 2022 saa 11 jioni baada ya kupigwa na mama yake mzazi, Jeska Balitazali.

Kamanda Mwampelwa amedai mama huyu alikuwa na desturi ya kumpiga mtoto huyo hadi kukimbia nyumba na kuhamia kwa majirani.

Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Nyancheche, Josephati Maumba ameeleza kuwa mtoto huyo alikuwa mwanafunzi wa darasa la awali katika shule hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live