Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba atupwa jela maisha kwa kumnajisi mwanaye wa miaka 6

Rape ED Baba atupwa jela maisha kwa kumnajisi mwanaye wa miaka 6

Sun, 28 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baba mmoja amehukumiwa kifungo cha maisha jela nchini Kenya baada ya mahakama kumpata na hatia ya kumnajisi bintiye wa miaka sita.

Wakati wa hukumu, Hakimu Mkuu Mwandamizi, Monica Maroro alisema kuwa kosa hilo ni la kinyama na halikubaliki kwa mujibu wa sheria.

"Mtoto mdogo aliyehusika alikuwa na umri wa miaka sita pekee na mshtakiwa alimchukua kwenye uwanja wa michezo kabla ya kumnajisi kinyama katika nyumba ya jirani iliyokuwa ikifanyiwa ukarabati," Maroro alisema.

Alisema badala ya mtuhumiwa kuonesha mapenzi ya baba kwa msichana huyo aliamua kumnajisi. Alisema kuwa ushahidi uliotolewa mahakamani unatosha kuthibitisha kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.

“Kutokana na ripoti ya matibabu iliyowasilishwa mahakamani, kulikuwa na ushahidi wa kutosha kumbainisha mshtakiwa kwenye kosa hilo. Kulikuwa na jeraha ili kuhakikisha ni kweli, "aliongeza.

Wakati wote wa kesi, baba huyo alikana kutenda kosa hilo, lakini baada ya hukumu alikiri. Baba huyo alisema yeye ni mtu wa familia na alikuwa akijuta. Alisema kuwa alikuwa raia wa mapenzi mema na akisamehewa hatatenda tena kosa hilo.

Kulingana na shtaka, mwanamume huyo anasemekana kutenda kosa hilo kwa tarehe tofauti kati ya Septemba 3 na Septemba 23 huko Kawangware kaunti ya Nairobi.

Alikabiliwa na shtaka la pili la kufanya kitendo kichafu na mtoto. Akitoa ushahidi wake kortini, mtoto huyo aliambia mahakama kuwa mshtakiwa alimrubuni alipokuwa akicheza na marafiki zake "Nilikuwa nacheza kwa uwanja akanichukua, akanipeleka kwa nyumba na akafanya tabia mbaya."

Msichana huyo alisema baada ya shambulio hilo, babake alimwambia asimwambie mtu yeyote, akiwemo mama yake, na kuahidi kuchukua "hatua nzito" ikiwa angethubutu kufanya hivyo.

Alisema kuwa aliamua kuzungumzia shambulio hilo na mama yake ambaye aliripoti haraka kwa polisi na kumfanya akamatwe. Mama wa mtoto huyo pia alitoa ushahidi mahakamani na kueleza jinsi alivyojua kuhusu tukio hilo.

Afisa wa uchunguzi alikuwa wa mwisho kutoa ushahidi kabla ya kesi kufungwa. Mshtakiwa aliiambia mahakama kuwa alikuwa mwathirika wa mazingira na shtaka dhidi yake lilikuwa na shaka.

Alisema kuwa maafisa wa polisi walimkamata usiku akiwa amelala pamoja na familia yake. Alishikilia muda wote wa kesi kwamba hakuwahi kutenda kosa hilo. Hata hivyo, hakimu alitupilia mbali utetezi wake na kusema kuwa alitenda.

Hakimu alimpa siku 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iwapo angetaka kufanya hivyo. “Baada ya kuzingatia upande wa mashitaka na utetezi, ninamhukumu mshtakiwa kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa hilo, ana siku 14 za kukata rufaa iwapo angependa kufanya hivyo,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live