Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba atuhumiwa kumbaka mwanaye

UBAKAJI Pia anadaiwa kuwabaka mabinti wengine wawili

Tue, 19 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoani Manyara linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Masakta wilayani Hanang', Simon Zacharia (58) kwa tuhuma za kumbaka mwanaye wa kumzaa (12).

Pia, anatuhumiwa kuwabaka mabinti wengine wawili kwa nyakati tofauti mmoja kwenye shamba la mahindi.

Akizungumza mapema hii leo Jumanne Aprili 19, 2022 Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa huo, Limited Mhongole amesema matukio hayo yametokea katika siku tofauti.

Kamanda Mhongole amesema mtuhumiwa huyo anadaiwa kufanya mapenzi na mwanaye ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba shambani na kumtisha kumuua endapo atatoa siri hiyo.

"Kabla ya hapo alishawahi kuwabaka mabinti wengine wawili kwa nyakati tofauti katika kijiji hicho," amesema kamanda Mhongele.

Amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakama upelelezi utakapokamilika.

Advertisement

Chanzo: www.tanzaniaweb.live