Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba asimulia mwanawe alivyouawa akiimba nyimbo za utukufu

40458 Babapic Baba asimulia mwanawe alivyouawa akiimba nyimbo za utukufu

Thu, 7 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mazishi ya Isaka Petro (28) anayesadikiwa kuuawa na mkurugenzi wa halmashauri ya Itigi yalifanyika jana nyumbani kwao Kijiji cha Kazikazi lakini waumini wamesimulia kuwa alikufa wakati akiimba.

Petro aliuawa kwa kupigwa risasi Jumamosi ya Februari 2,2019 na kuzikwa jana baada ya utata wa kifo chake ambapo mazishi yake yaliongozwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo aliyetoa ubani wa Serikali wa Sh1 milioni.

Baba mzazi wa Isack, Petro Chambalo amesema uwanja wa kanisa siku hiyo uligeuka kuwa vita na milio ya bunduki na kwamba walijua dunia imekwisha.

"Lakini mwanangu alikufa akiimba nyimbo za utukufu, yeye hakujibu kitu zaidi ya kuamua wakati mkurugenzi na mtendaji wa kijiji walipokuwa wanamtoa muumini nje," amesema Petro.

Amesema siku hiyo marehemu alikuwa anaongoza ibada kwa kuwa alikuwa ni msaidizi wa mchungaji na katika ibada hiyo mchungaji hakuwepo.

Soma Zaidi: Baba aeleza alivyoshuhudia mwanaye akipigwa risasi kanisani

 

Soma Zaidi: Jafo alaani matumizi ya nguvu kubwa kwa raia



Chanzo: mwananchi.co.tz