Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba amuua mtoto wake kwa shoka akigombana na mkewe

Shokazzz.jpeg Baba Amuua Mtoto Wake Kwa Shoka Akigombana Na Mkewe

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mwanaume aitwaye Anderson Clemence (35), mkazi wa kijiji cha Kafunjo, Kata ya Kamagambo wilayani Karagwe kwa tuhuma za kumuua mtoto wake Hansen Anderson, mwenye umri wa miezi minne kwa shoka.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Wankyo Nyigesa, amesema kuwa baba huyo alikamatwa Machi 01, 2022 na kwamba chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi baina yake na mke wake.

Amesema kuwa wakati wakigombana mtuhumiwa alirusha shoka ili kumpiga mke wake na badala yake likampiga mtoto huyo aliyekuwa amebebwa mgongoni na mama yake mzazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live