Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba amuua bintiye kwa kipigo

10970 Kipigo+pic TanzaniaWeb

Thu, 9 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Misungwi.  Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Sumbugu wilayani hapa Mkoa wa Mwanza, Mariamu Tabu amefariki dunia kwa madai ya kupigwa na baba  baada ya kutohudhuria shuleni.

Akizungumza leo Agosti 9, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kituo cha Misungwi na atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka.

Mama mzazi wa Mariam, Kija Mashauri  amesema Agosti 6, mwanaye alikwenda shule lakini hakurudi nyumbani badala yake alirudi Agosti 7 jioni.

“Aliporudi baba yake alimuuliza alipokuwa na kuanza kumpiga kwa mchi (mtwangio), wakati akimpiga niliona kipigo hicho ni kikubwa nikaenda kuomba msaada kwa jirani ambaye ni mwenyekiti wa kijiji (Samweli Mtobela).

“Mume wangu alitaka kukimbia lakini walimkamata na kumpeleka mtoto zahanati ya Sumbugu kisha kituo cha afya cha Mbarika, wakiwa njiani wanakwenda mwanangu alifariki dunia.”

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mtobela amesema mtoto huyo alifariki dunia akiwa  mapokezi kwenye kituo cha afya huku baba yake akiwa chini ya ulinzi.

“Tulimpeleka mtuhumiwa kituo cha polisi na kurudisha mwili nyumbani,”amesema.

Mwalimu mkuu msaidizi wa Sekondari ya Sumbugu, Vincent Mugunga amesema Mariamu alikuwa kidato cha nne na kwamba kwa mujibu wa daftari la mahudhurio hakufika shuleni tangu Julai 30 mwaka huu.

Amesema baba yake alifika shuleni hapo Agosti 6 kumuangalia lakini hakumkuta.

Chanzo: mwananchi.co.tz