Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba adaiwa kumuua mwanaye kisa kulialia

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Geita, Safia Jongo.jpeg Baba adaiwa kumuua mwanaye kisa kulialia

Fri, 12 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja mkazi wa mtaa wa Kilimahewa, Mamlaka ya mji mdogo wa Katoro wilayani Geita, Kubilu Mahege (20) amemuua kwa kumpiga mwanaye mchanga kutokana na ugomvi wa kifamilia.

Mama mzazi wa marehemu, Riziki Leonard, amesema mumewe alimpiga mtoto makofi pamoja na kumchapa kwa mkanda wa suruali katika maeneo mbalimbali mwilini mwake baada ya kuona (mtoto) analia usiku.

Kwa upande wake Mtendaji wa Mtaa wa Kilimahewa, Marko Chuma, amesema mtuhumiwa wa mauji hayo alitoroka baada ya kutekeleza mauji.

Wakati anakula, mtoto alianza kulia, na mama akabaki akitoa vyombo mezani na ndipo mume wake alienda kitandani kumuangalia alikokuwa amelala akamtoa mtoto kitandani na kumbeba kifuani huku akimnyamazisha lakini baadaye alianza kumpiga makofi ya mashavuni na mbavuni akimwambia anyamaze.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Safia Jongo amethibitisha tukio hilo na akieleza lilitokea Januari 11, 2024 majira ya saa saba usiku eneo lijulikanalo kama Kigamboni.

Kamanda Jongo amemtaja mtoto ambaye kwa sasa ni marehemu ni, Leonard Kubilu mwenye umri wa miezi mitano ambapo alifariki baada ya kupigwa kwa kutumia kiatu cha kike na mkanda na baba mzazi.

“Chanzo cha tukio hili ni ugomvi wa kifamilia na huyu baba alitoweka mara tu baada ya kufanya tukio hili lakini juhudi zinafanyika za kumtafuta mtuhumiwa.

“Kutokana na tukio hili nitoe wito kwa jamii kumrudia Mungu kwa sababu nikiangalia tukio kama hili hata kama kuna ugomvi, mtoto wa miezi mitano hajui hata kuongea alimkosea nini huyu baba.

“Kwa hiyo ni kama ni ugomvi kati ya mama na baba, sasa inakuaje ugomvi wa baba na mama unapelekea machungu kwa mtoto, mtoto anahusika na nini,” amesema Kamanda Jongo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live