Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba adaiwa kumlawiti mwanaye wa miaka mitano

Sat, 22 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Melon Joseph (25) mkazi wa Nyarugusu wilayani Geita mkoani hapa anadaiwa kumlawiti mwanaye mwenye umri wa miaka mitano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitishwa tukio hilo na kubainisha kuwa mhusika ameshakamatwa na polisi.

Akizungumza leo Jumamosi Septemba 22, 2018, Mwabulambo amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa mtoto huyo amefanyiwa unyama huo.

Amesema mhusika huyo amegundulika Septemba 18, 2018 wakati jirani yake akimuogesha mtoto huyo na kubaini kuwa ana maumivu sehemu za siri.

Kamanda huyo amebainisha kuwa wanaendelea na uchunguzi na ikibainika ni kweli mtoto huyo amefanyiwa unyama huo, sheria itachukua mkondo wake iwe fundisho kwa wengine.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz