Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba adaiwa kumchoma mwanae kwa upanga wa moto

49911 PANGQA+PIC

Tue, 2 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Mkazi wa mtaa wa Fisi, kata ya Igunga mjini mkoani Tabora, Nyalagi Simon amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Igunga kwa tuhuma za kumuunguza mwanae kwa upanga wa moto.

Simon amefikishwa leo Jumatatu Aprili 1, 2019 katika mahakama hiyo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya, Lydia Ilunda.

Mwendesha mashtaka wa Polisi, Ellymajid Kweyamba alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo saa tatu usiku Machi 17, 2019.

Amesema siku hiyo, mshitakiwa akiwa baba wa mtoto (jina linahifadhiwa) alimfanyia vitendo vya ukatili kwa kutumia upanga aliouweka kwenye moto.

Amebainisha kwamba mshitakiwa alikuwa akiutoa upanga kwenye moto na kumuunguza kwenye miguu yote miwili.

Mshitakiwa amekana shitaka lake na amepelekwa mahabusu hadi Aprili 14, 2019 shauri lake litakapotajwa tena.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz